Browse images and videos on Instagram. Find out Most Popular Hashtags and Users.imgable
 1. Homepage
 2. @storynzuriiplanet
Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet
Fullname

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Bio 🔵East African Artist 🔥Mr Romantic TANZANIANBOY🇹🇿 Subscribe YouTube channel (storynzuriiplanet) 👇👇👇👇👇

Profile Url

Share
Statistics for "Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)"
Suggested users for Instagram Profile "Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)"
HamisaMobetto (@hamisamobetto) Instagram Profile Photohamisamobetto

HamisaMobetto

Irene Uwoya (@ireneuwoya8) Instagram Profile Photoireneuwoya8

Irene Uwoya

Chibu Dangote..! (@diamondplatnumz) Instagram Profile Photodiamondplatnumz

Chibu Dangote..!

Wema Sepetu (@wemasepetu) Instagram Profile Photowemasepetu

Wema Sepetu

Idris Sultan (@idrissultan) Instagram Profile Photoidrissultan

Idris Sultan

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram photos and videos

List of Instagram medias taken by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet)

Browse image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 21
MTUNZI:EDO MAN “Leo lazima kieleweke, siondoki mpaka nizungumze naye,” alijisemea Ibrahim.
Daki" - 1958099629439781320
ReportShareDownload154

HADITHI:MREMBO LATIFA 21 MTUNZI:EDO MAN “Leo lazima kieleweke, siondoki mpaka nizungumze naye,” alijisemea Ibrahim. Dakika ziliendelea kusonga mbele huku wanafunzi wakiendelea kutoka, alikuwa kama mtu anayewahesabu wanafunzi hao, mpaka mwanafunzi wa mwisho anatoka ndani ya ndani ya shule, Latifa hakuwepo. “Mmmh! Hajafika au alipita ila sikumuona?” alijiuliza Ibrahim. Hakutaka kuvumilia kusimama nje, alichokifanya ni kuelekea ndani ya shule ile na kukutana na walinzi, akaanza kuwauliza kuhusu Latifa, kwa sababu alikuwa maarufu, halikuwa tatizo. “Hauna habari nini?” aliuliza mlinzi mmoja. “Habari gani?” Ibrahim aliyasikia mapigo ya moyo wake yakidunda kwa nguvu, hofu ikamuingia, akajikuta akianza kusali kimoyomoyo mlinzi yule asimpe taarifa mbaya kuhusu Latifa kwa kuamini kwamba moyo wake ungemuuma sana. “Latifa alipata ajali asubuhi, nimesikia hali yake mbaya sana, aligongwa na gari hapo Jangwani na amepelekwa hospitalini huku akiwa hajitambui. Tetesi zinasema kwamba anatakiwa kusafirishwa kupelekwa India kwa matibabu zaidi,” alisema mlinzi yule, Ibrahim akachanganyikiwa. “Unasemaje?” aliuliza Ibrahim kwa mshtuko. “Ndiyo hivyo, yaani leo watu wamemmisi sana, si unajua alivyokuwa mkali,” alisema mlinzi yule. Ibrahim hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alihisi kuchanganyikiwa, alichokifanya ni kuanza kutimua mbio kuelekea Muhimbili kumwangalia, alionekana kama chizi, mapenzi yaliuendesha moyo wake vilivyo. **** Ulisikika mlio mkubwa wa gari, watu wakapiga mayowe, wengine wakashika vichwa vyao, hawakuamini walichokiona, msichana mdogo aliyevalia sare za shule aligongwa na gari, alirushwa juu, akazungushwa, alipotua chini, hakutingisha, akatulia tuli. Damu zilimtoka mfululizo, shati lake jeupe alilolivaa, ilikuwa vigumu kujua kama lilikuwa jeupe au jekundu, lilitapakaa damu hali iliyoonyesha kwamba msichana huyo alikuwa ameumia vibaya. Watu waliokuwa pembezoni mwa barabara wakaanza kumfuata, dereva aliyekuwa amemgonga, hakukimbia, akateremka na kumfuata mahali pale alipoangukia. Kila mtu aliyemuona msichana huyo, alishika kinywa chake kwa mshtuko, kwa muonekano, msichana yule alionekana kufariki dunia palepale.

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 20
MTUNZI:EDO MAN

Hisia kali za mapenzi juu ya msichana huyo zikamtawala, kila alipokaa, alimfiki" at Kigamboni Bridge - 1958098489134355880

HADITHI:MREMBO LATIFA 20 MTUNZI:EDO MAN Hisia kali za mapenzi juu ya msichana huyo zikamtawala, kila alipokaa, alimfikiria Latifa na hata katika kipindi cha kuondoka shuleni hapo, hakuwa tayari kuondoka mpaka pale alipomuona msichana huyo. Kwa mwaka mzima Ibrahim aliendelea kumfuatilia Latifa, hakuwahi kuzungumza naye, alimuogopa, ni mara nyingi alipanga kumfuata lakini kila alipotaka kumsogelea, mapigo yake ya moyo yalidunda mno na hofu kumjaa. Wavulana wengine walimfuata Latifa lakini mwisho hakukuwa na mvulana yeyote aliyekubaliwa. Kila alipowaangalia wavulana waliomfuata Latifa na kujiangalia yeye, alijiona kutokuwafikia hata mara moja. Hakuwa mvulana tajiri, alitoka katika familia masikini ambayo haikuwa na mbele wala nyuma. Ibrahim alikuwa kama Latifa, japokuwa alikuwa kijana masikini lakini alikuwa na uwezo mkubwa darasani, katika kila mtihani aliofanya, aliongoza kwa maksi nyingi kiasi kwamba alikuwa gumzo kwa walimu wote. “Nataka kuwa daktari, ila daktari bila kuwa na mke mrembo haiwezekani, Latifa atanifaa,” alisema Ibrahim. Moyo wake uliendelea kuumia kila siku, kumfuata Latifa na kumwambia ukweli aliogopa sana. Mwaka mwingine ukaingia na kupita, mwaka wa tatu ulipoingia, Ibrahim akashindwa kuvumilia, hakuwa tayari kujiona akiteseka na wakati kulikuwa na mtu ambaye angeweza kuyatuliza mateso yake ya moyo. Siku hii alikuwa amejipanga vilivyo, alivalia nadhifu huku akiwa amevipiga kiwi viatu vyake. Aliipanga siku hiyo kuwa maalumu kuzungumza na msichana huyo, kumwambia kila kitu kilichokuwa kikiusibu moyo wake. Baada ya kufika shuleni, hakutaka kutoka darasani, alivumilia mpaka muda wa kutoka. Kadiri muda ulivyozidi kwenda mbele, mapigo yake ya moyo yakawa yanaongeza kasi ya udundaji, alipenda kuonana na Latifa lakini moyo wake ulijawa hofu kubwa. Baada ya kengele kutoka, moja kwa moja akaelekea nje ya shule na kusimama barabarani. Macho yake yalikuwa katika geti la shule ile ya wasichana, alikuwa akimsubiria Latifa tu. “Leo lazima kieleweke, siondoki mpaka nizungumze naye,” alijisemea Ibrahim. Dakika ziliendelea kusonga mbele huku wanafunzi wakiendelea kutoka, alikuwa kama mtu anayewahesabu wanafunzi hao,

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 19
MTUNZI:EDO MAN

Uwezo wake huo ukawashangaza walimu wote, hawakuamini kama kungekuwa na mtoto a" at Dar es Salaam, Tanzania - 1957520943095232078

HADITHI:MREMBO LATIFA 19 MTUNZI:EDO MAN Uwezo wake huo ukawashangaza walimu wote, hawakuamini kama kungekuwa na mtoto ambaye angeweza kufanya vitu hivyo kwa haraka kama alivyokuwa Latifa. Hata mitihani ya shuleni hapo ilipokuwa ikija, Latifa alikuwa akiongoza jambo lililowafanya walimu kumpeleka darasa jingine la juu kwani uwezo wake ulikuwa ni wa kitofauti kabisa. Kwa kifupi tungesema Latifa alikuwa genius. Mpaka anaanza darasa la kwanza, Latifa alikuwa mtoto mwenye uwezo mkubwa darasani, katika kila mtihani, alikuwa akifanya vizuri kitu kilichowashangaza sana walimu kwani hakukuwa na mwanafunzi yeyote aliyewahi kusoma shuleni hapo huku akiwa na akili nyingi kama Latifa. Mbali na uwezo wake darasani, Latifa alikuwa mtoto mrembo ambaye usingeweza kumwangalia mara moja na kuyaamisha macho yako. Mchanganyiko wake wa rangi ulivichanganya vichwa vya watu wengi kiasi kwamba wengine wakatabiri kuwa angekuwa miongoni mwa wasichana watakaoitikisa Tanzania. Miaka ilikatika zaidi, mpaka Latifa anaingia kidato cha kwanza katika Shule ya Wasichana ya Jangwani, uzuri wake uliendelea kuwatikisa watu wengi wakiwepo wavulana waliokuwa wakisoma katika Shule ya Wavulana ya Azania. “Kuna demu nimekutana naye, ni mkali balaa, anasoma hapo Jangwani, aisee huyo demu ni shida,” alisikika mwanafunzi mmoja akiwaambia wenzake. “Yupo vipi?” “Muhindi si Muhindi, Mswahilini si Mswahili, ni noma.” “Hahaha! Utakuwa unamzungumzia Latifa.” “Latifa! Latifa yupi?” “Kuna msichana wa kidato cha kwanza, ni mzuri ile mbaya, halafu ana akili kinoma,” alisema mwanafunzi mwingine. Stori juu ya uzuri wa Latifa ndizo zilizokuwa zikisikika, uzuri wake uliendelea kumdatisha kila aliyemwangalia. Watu wakazidi kuambiana kuhusu Latifa kiasi kwamba binti huyo akaanza kupata umaarufu katika shule hizo mbili. **** Miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wakimpenda Latifa alikuwa Ibrahim Musa, kijana mtanashati aliyekuwa akisoma katika Shule Wavulana ya Azania. Kila siku alipokuwa akisikia stori kuhusu Latifa, Ibrahim alihisi moyo wake ukitetemeka kwa mahaba mazito. Hisia kali za mapenzi juu ya msichana huyo zikamtawala, kila alipokaa, alimfikiria Latifa

Browse image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 18
MTUNZI:EDO MAN

Kitendo alichokifanya Nahra cha kukubali kuzaa na mtu mwenye ngozi nyeusi, Deo " - 1957445685428571789
ReportShareDownload353

HADITHI:MREMBO LATIFA 18 MTUNZI:EDO MAN Kitendo alichokifanya Nahra cha kukubali kuzaa na mtu mwenye ngozi nyeusi, Deo kiliwachukiza mno, hawakutaka kumuona, hawakumpenda na hata hawakutaka kuufikiria uzao wake, kwao, uzao wa Nahra ukawa ni uzao wenye laana. Baada ya kila kitu kumalizika na Nahra kuzikwa, Issa akawa na jukumu kubwa na zito la kumlea mtoto Latifa. Kila alipomwangalia, moyo wake ulimuuma mno kwani sura yake ilimkumbusha Nahra. “Wazazi wa Nahra wana roho mbaya sana, wamemkataa Nahra na uzao wake wote,” Issa alimwambia dada yake, Semeni aliyekuwa na jukumu la kukaa na Latifa. “Kisa? Kazaa na mtu mwenye ngozi nyeusi, ni hatari sana.” Latifa alikuwa mtoto mkimya, hakuwa mtoto wa kulialia kama ilivyokuwa kwa baadhi ya watoto. Hakukuwa na shida ya kumlea, kwa Semeni, alimchukulia kama mtoto wake wa kumzaa, huduma zote alizokuwa akiwapa watoto wake wa kuwazaa, alikuwa akimpa Latifa pia. Mwaka wa kwanza ukakatika na wa pili kuingia, Latifa aliendelea kukua huku uzuri aliokuwa nao ukiendelea kuonekana zaidi, ulipofika mwaka wa pili, watu wakaanza kupigishana kelele kwa kudai kwamba Latifa angeweza kuwa mwanamke mrembo kuliko wanawake wote duniani, uzuri wake ulimdatisha kila mtu. “Aiseee! Kama malaika!” alisema jamaa mmoja. “Kwani ushawahi kumuona malaika?” jamaa mwingine akauliza huku akicheka. “Sijawahi, lakini huyu kama malaika, amini hilo.” Uzuri wa Latifa ukawa gumzo Manzese nzima, kila aliyekuwa na hamu ya kutaka kumuona mtoto mzuri alikuwa akiambiwa kwenda nyumbani kwa Semeni kumuona Latifa. Mwaka wa tatu ulipoingia, Latifa akaanzishwa shule ya chekechea. Miongoni mwa watoto waliokuwa wakimya, Latifa alikuwa mmojawapo, hakuwa mzungumzaji kabisa, hakuwa mtundu, alipokuwa akikaa muda huu, hadi muda wa kutoka alikuwa hapohapo. Mbali na ukimya wake, walimu wakagundua kitu kimoja kwamba Latifa hakuwa mtoto wa kawaida, uwezo wake darasani ulikuwa ni wa juu mno. Yeye ndiye alikuwa mwanafunzi wa kwanza kujua kusoma na kuandika japo kwa mwandiko mbaya. Uwezo wake huo ukawashangaza walimu wote, hawakuamini kama kungekuwa na mtoto ambaye angeweza kufanya vitu hivyo kwa haraka kama alivyokuwa Latifa.

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 17
MTUNZI:EDO MAN

Huo ukawa muendelezo wa mateso aliyoyapata, mara kwa mara alikuwa akiletewa mto" at Dar es Salaam, Tanzania - 1957441854334539689

HADITHI:MREMBO LATIFA 17 MTUNZI:EDO MAN Huo ukawa muendelezo wa mateso aliyoyapata, mara kwa mara alikuwa akiletewa mtoto wake na kuanza kumwangalia, moyo wake ulimuuma, alikuwa akiyauma meno yake kwa hasira na kuwapa lawama zote wazazi wake na Deo ambao walimfanya kuwa hapo. Kila kitu kikabadilika, mtu pekee aliyekuwa akiyaangalia maisha yake ya mateso kitandani pale alikuwa Issa tu. Siku zikakatika, mwili wake ulizidi kukonda na vipele kuongezeka, kwa kumwangalia tu, usingebaki kimya, machozi yangekulenga na kusema kwamba Nahra alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakipitia mateso makali. “Issa, kama nitakufa, naomba umsomeshe mtoto wangu mpaka chuo kikuu,” alisema Nahra huku akionekana kukata tamaa. “Usijali, nitajitahidi, hata kama nitakosa fedha, nitakopa tu.” “Issa, nilikwishawahi kukuelekeza nyumbani, si ndiyo?” “Ndiyo.” “Utaweza kupakumbuka?” “Nafikiri nitaweza.” “Basi hapo ndipo utakapotakiwa kwenda endapo utapata tatizo lolote kuhusu fedha,” alisema Nahra. “Wataweza kunisaidia kweli?” aliuliza Issa. “Watakusaidia tu, huyu ni mjukuu wao na si mtoto wao, hana kosa, watakusaidia tu, amini hilo.” “Sawa, nitajaribu japokuwa sina uhakika, nikipata tatizo, nitakwenda huko, nisipopata, hawatoniona,” alisema Issa ambaye kila alipomwangalia Nahra, moyo wake ulimuuma mno. Siku hiyo Nahra aliongea kwa shida sana, ilipofika saa saba mchana, mateso aliyokuwa akiyapata kitandani yakaisha na kukata roho. Huo ukawa msiba mkubwa kwa Issa, alibaki akilia sana lakini machozi yake hayakuweza kubadilisha kitu chochote kile, Nahra alifariki kwa Ugonjwa wa UKIMWI. Alichokifanya Issa ni kuelekea nyumbani kwa kina Nahra, japokuwa alielekezwa juu kwa juu lakini alifanikiwa kufika huko. Mtu wa kwanza kabisa kumpa taarifa za msiba alikuwa mlinzi wa getini, Chichi ambaye aliwapelekea taarifa wazazi wake Nahra. “Acha afe, tulimwambia azae na mtu mweusi,” alisema mzee Patel, Mhindi aliyekuwa na roho mbaya. Japokuwa Wahindi wengine walipewa taarifa kuhusu msiba wa Nahra lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyejitokeza kwenda huko, walibaki majumbani mwao wakiendelea kuyafurahia maisha. Kitendo alichokifanya Nahra cha kukubali kuzaa na mtu mwenye ngozi nyeusi,

Browse image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 16
MTUNZI:EDO MAN

Afya yake iliendelea kuzorota huku vipele vikiendelea kumsumbua mwilini mwake.
" - 1957201650797338524
ReportShareDownload258

HADITHI:MREMBO LATIFA 16 MTUNZI:EDO MAN Afya yake iliendelea kuzorota huku vipele vikiendelea kumsumbua mwilini mwake. “Twende hospitali,” alisema Issa. “Hapana. Siwezi kwenda.” “Kwa nini?” “Naogopa sindano.” “Hapana. Utakwenda tu.” Afya ilikuwa yake lakini kwenda hospitali ilikuwa mbinde. Alichokifanya Issa ni kumbeba na kuanza kuondoka naye kinguvu. Muda wote Nahra alikuwa akilalamika kwamba hakutaka kwenda hospitalini lakini Issa hakujali, aliendelea kumbeba mpaka walipofika katika Hospitali ya Halmashauri, Tandale. “Apelekwe Muhimbili kwa vipimo zaidi,” alisema daktari mwenye sura ya upole na huruma, Dk. Mariamu. Issa hakuchoka, kwa sababu alikuwa na kiasi fulani cha fedha, akachukua bajaji na safari ya kuelekea Muhimbili kuanza. Walipofika huko, vipimo vikachukuliwa na Nahra kuonekana kuwa na ugonjwa hatari wa UKIMWI. Hiyo ilikuwa taarifa mbaya kwake, msichana aliyekuwa na mvuto kiasi cha kuwatetemesha wanaume wengi, leo hii alikwisha kabisa na kuambukizwa ugonjwa hatari wa UKIMWI. Nahra alilia sana lakini kilio chake hakikubadilisha kitu, mtu pekee aliyekuwa akimfariji alikuwa Issa tu. Siku zikaendelea kukatika, vipele vikaongezeka mwili huku ukiendelea kupungua mpaka kufikia hatua ya kuanza kupata mabakabaka fulani mwisho wa siku nywele zake kuanza kunyonyoka, zote hizo zilikuwa dalili za ugonjwa hatari wa UKIMWI. Nahra aliendelea kuisha, aliharibika na kila siku alikuwa mgonjwa. Japokuwa kila siku alitamani sana kwenda klabuni kulewa lakini kwa hatua aliyofikia, hakuwa na nguvu za kuweza kusimama. Akawa mtu wa ndani tu. “Ninakufa Issa, ninataka kumuona mtoto wangu,” alisema Nahra huku akitia huruma kitandani. Issa hakuwa na cha kufanya, ni kweli kwa muonekano aliokuwa nao alionekana kutokuwa na muda mrefu kuendelea kuishi, alichokifanya ni kwenda kumchukua Latifa na kumletea. Alikuwa amefanana naye kwa kila kitu kuanzia uzuri na hata ngozi ya mwili. Nahra alibaki akimwangalia mtoto wake tu, machozi yakaanza kumbubujika mashavuni pale alipokumbuka kwamba alikuwa mfu aliye hai. Huo ukawa muendelezo wa mateso aliyoyapata, mara kwa mara alikuwa akiletewa mtoto wake na kuanza kumwangalia, moyo wake ulimuuma,

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 15
MTUNZI:EDO MAN “Wewe mwanamke, utamuua huyo mtoto! Unampa gongo!” alisema mlevi mmoja, alikuwa " at Kurasini, Dar Es Salaam, Tanzania - 1957198235761555090

HADITHI:MREMBO LATIFA 15 MTUNZI:EDO MAN “Wewe mwanamke, utamuua huyo mtoto! Unampa gongo!” alisema mlevi mmoja, alikuwa akimwangalia Nahra kwa mshangao. “Achana na mimi, usifuatilie maisha yangu, fanya kilichokuleta,” alisema Nahra huku akiona kila kitu alichokuwa akikifanya kuwa sawa. Walevi wengine hawakupenda kuona jambo hilo likiendelea kutokea, walichokifanya ni kumwambia Issa ambaye alionekana kuchukizwa na kitendo hicho na hivyo kumchukua Latifa na kumpeleka kwa dada yake, Semeni aliyekuwa akiishi Manzese Midizini. Pombe zilizidi kumkolea Nahra, wakati mwingine hakuwa akirudi kabisa nyumbani, pombe zilimkolea na kulala hukohuko klabuni. Issa alikuwa kwenye wakati mgumu, japokuwa alimchukua mwanamke huyo kwa ajili ya kumsaidia lakini kwa kipindi hicho, kwa kiasi fulani alikuwa akijuta. Kila siku ilikuwa ni lazima kumfuata Nahra klabuni na kumrudisha nyumbani, japokuwa lilikuwa zoezi gumu kwake lakini hakuwa na jinsi, alifanya kila kinachowezekana kuhakikisha Nahra analala nyumbani kwake. Mwaka wa kwanza ukakatika, Nahra aliendelea kubaki katika hali ya ulevi mkubwa, na mpaka mwaka wa pili unaingia, tayari alikuwa mnywaji mkubwa kuliko wanywaji wote waliomtangulia. “Mtoto wangu yupo wapi?” aliuliza Nahra, mwili wake ulikuwa umekonda mno huku ukiwa na vipele vingi. “Yupo kwa dada yangu. Ameanza shule, usihofu kitu chochote kile,” alijibu Issa. “Nataka kumuona mtoto wangu,” alisema Nahra kwa staili ya kulalamika. “Utamuona tu. Usijali.” “Lini?” “Wewe unataka lini?” “Leo.” “Kwa leo haitawezekana. Tufanye keshokutwa,” alisema Issa. Siku ziliendelea kukatika, Issa hakutaka kumruhusu Nahra kumuona mtoto wake. Alijua fika kwamba alifanya makosa lakini alijaribu kuepuka matatizo ambayo yangeweza kutokea endapo tu mwanamke huyo angekutana na mtoto wake. Nahra hakuacha kumuulizia Latifa, kila siku ilikuwa ni lazima amuulize Issa kuhusu mtoto wake na jibu lake lilikuwa lilelile kwamba angekwenda naye Manzese kumuona. Mwezi wa kwanza ukakatika tangu amuulizie Latifa, mwezi wa pili na wa tatu ikakatika na hatimaye mwaka mzima kukatika. Afya yake iliendelea kuzorota huku vipele vikiendelea kumsumbua mwilini mwake. “

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI: MREMBO LATIFA 14

MTUNZI:EDO MAN

Baada ya miezi tisa kutimia, Nahra akajifungua mtoto mzuri wa kike ambaye ali" at Dar es Salaam, Tanzania - 1956064035922591821

HADITHI: MREMBO LATIFA 14 MTUNZI:EDO MAN Baada ya miezi tisa kutimia, Nahra akajifungua mtoto mzuri wa kike ambaye alimpa jina la Latifa. Japokuwa alikuwa mtoto mdogo, uzuri wa sura yake haukuweza kujificha, alipokuwa akicheka, akitabasamu na hata kulia, bado uzuri wake ulikuwa palepale. “Amechukua sura yako, mmmh! Katoto kazuri,” alisema Issa huku akimwangalia Latifa. “Ahsante.” “Kwa hiyo ndiyo baba yake alimkataa?” “Ndiyo.” “Duuh! Makubwa.” Kila alipomwangalia mtoto wake, Latifa, Nahra aliumia, mawazo juu ya Deo yakaanza kumtawala. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali hakuamini kama mtoto aliyekuwa amezaliwa alikataliwa na mwanaume aliyezaa naye. Siku zikakatika na mawazo kuzidi kumuumiza. Latifa alipofikisha kipindi cha miezi miwili tu, Nahra akaanza kuvuta sigara na kunywa pombe za kienyeji, hakufanya hayo kwa kuwa alipenda, alijitahidi kuyaondoa mawazo juu ya Deo kwa kuwa mlevi na mvutaji. Sigara na pombe ya kienyeji, gongo hazikumpenda, ghafla, tena ndani ya miezi mitatu tu, afya yake ikaanza kubadilika, mwili ukaanza kupungua na vipele kuanza kumtoka. Afya ikazidi kudhoofika zaidi, na mwisho wa siku, akabaki mifupa mitupu, gongo aliyokuwa akiinywa, iliuteketeza mwili wake. Mwili uliendeea kupungua kila siku, sehemu yake kubwa aliyokuwa akiishi kwa wakati huo ilikuwa klabuni tu. Japokuwa Issa alikuwa mlevi na mvutaji sigara mzuri lakini kwa Nahra alionekana kuwa zaidi yake. Uzuri wake haukupungua japokuwa mwili wake ulichoka mno kutokana na unywaji wa pombe za asili na uvutaji sigara. Maisha yake yakazidi kupoteza dira, wale waliokuwa wakimfuatilia, hawakumfuatilia tena, walevi aliokuwa akinywa nao klabuni ndiyo waliopata nafasi ya kumchukua na kufanya naye mapenzi. Kwa sababu hakuwa na fedha, mlevi yeyote yule aliyemsaidia kiasi cha shilingi mia tano kwa ajili ya kununua kikombe kimoja cha gongo, naye alikuwa akimuweka kwenye foleni ya kufanya naye mapenzi usiku ndani ya choo cha klabuni hapo. Kwa Latifa, hakupokea malezi bora, kila siku aliachwa nyumbani na hata kama ilitokea siku mama yake kumchukua na kwenda naye klabuni, alipolilia maziwa, alipewa kiasi cha pombe kunywa. “Wewe mwanamke, utamuua huyo mtoto! Unampa gongo!”

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 13
MTUNZI:EDO MAN “Ndiyo hivyo. Mzee katili sana, alimfukuza kama hamjui. Hapa unaweza kuniletea m" at Ilala, Dar Es Salaam, Tanzania - 1956061655990787506

HADITHI:MREMBO LATIFA 13 MTUNZI:EDO MAN “Ndiyo hivyo. Mzee katili sana, alimfukuza kama hamjui. Hapa unaweza kuniletea msala, mzee akikuona anaweza kukuua na kunifukuza kazi, kama vipi wewe jiachie tu,” alisema Chichi. “Sawa. Haina noma, niende wapi sasa? Nikamtafutie wapi?” “Sijajua. Popote pale wewe nenda tu,” alisema Chichi, akaingia ndani na kufunga geti. Deo akabaki nje, alichanganyikiwa, hakujua ni wapi alitakiwa kuanzia kumtafuta msichana wake, bado alichanganyikiwa mno na hakujua mahali alipokuwa msichana wake aliyekuwa na ujauzito wake. Hakuwa na jinsi, kwa sababu alitakiwa kuondoka na hapo nyumbani ndiyo sehemu pekee ambayo aliamini angeweza kumkuta Nahra, akaondoka zake na kurudi nyumbani huku uso wake ukiwa na huzuni mno. ***** Maisha hayakuwa ya kawaida, kuishi na mtu ambaye hakuwa na malengo yoyote yale zaidi ya kuendekeza pombe na kuishi kwa kuuza vyuma chakavu, yalikuwa maisha magumu mno. Issa hakuwa mwanaume aliyekuwa akimhitaji, lakini kwa wakati huo, hakuliangalia hilo, aliona ni bora kuishi naye hivyohivyo tu kwani hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda, kama kwa mpenzi wake, alifukuzwa, kwa wazazi wake ndiyo kabisa hawakutaka kabisa kumuona, hivyo hapo kwa Issa kulionekana kuwa msaada mkubwa wa maisha yake. Tofauti na matarajio yake, Issa hakumtaka kimapenzi hata siku moja, kila siku walikuwa wakilala wote lakini hakukuwa na siku aliyokuwa akimgusa kitu kilichomfanya Nahra kufikiria vibaya. Marafiki wa Issa hawakukauka, uzuri wa Nahra ulikuwa gumzo mtaani, kila wakati, wanaume walifika nyumbani hapo na mtu pekee waliyekuwa wakitaka kumuona alikuwa Nahra tu. Issa alikuwa mkali kwa kila mwanaume aliyemtaka Nahra, hakutaka mtu yeyote amuingilie msichana huyo na wakati alikuwa kwenye ngome yake. Wapo waliokuwa wakimfuata kwa pesa ili awaunganishie wawe naye lakini vyote hivyo, Issa aliendelea kukataa. Siku ziliendelea kukatika, miezi ikasonga mbele mpaka tumbo la Nahra kuanza kuonekana. Hapo, Issa aliendelea kuhangaika zaidi, hakutaka kukaa nyumbani, alijitahidi kutoka kwenda mihangaikoni ili kuhakikisha kwamba chakula kinapatikana cha kutosha kwa ajili ya Nahra aliyekuwa mjauzito.

MWANAUME NI MWANAUME 😂🤣 *MANENO KUNTU* . Mtu kwa muda mfupi tu anabadilika kutoka "Nakupnd sana" kwenda "nakuchkia sana". Anakufanya unajisikia vizuri kidogo tu anakunadilikia..ni mbaya zaidi kama umzaa na mtu wa aina hiyo ambae haeleweki. Huu upzi wa kutokueleweka kwenye mahucan ni utoto. Mtu ambae amekua kiakili anahitaji uhakika. Mtu aliyekua kiakili anaeleza wazi kama mahucan yapo au hayapo. Kuwa na uhakika na maamuzi yako kuliko kupotezeana muda. Acha kumchzea michezo ya kitoto mwenzak. Chagua moja kama upo kwenye uhucano nae au laa. Usiwe mguu mmoja ndani mguu mmoja nje. Mapnz sio moody. Mapnz ni kitu ambacho kipo constant. Mapnz yanatabirika na yanayotegemeana. Mapnz ni facts sio theory. Mpe mtu clarity kuhusu mahucano yenu. Ndoa imara na Mahucano imara hayajengwi kwa misingi ya mapnz yasiyo na uhakika. Mtu uliyenae anaweza kabisa kukubaliana na matokeo. Kama haumtaki tena mweleze wazi ili afahamu amesimama wapi. Ni bora kukataliwa sasa hivi ukaendelea na maisha yako huku ukijitahidi kutibu moyo, kuliko kuendelea kusaltwa na mtu ambae hafahamu ni nini anachokitaka...

WA KISASA @carrymastory@idrissultan@hamisamobetto@diamondplatnumz@officialalikiba@divatheebawse *MANENO KUNTU -----///////////(((/(//// .. Hakuna kitu kinachoudhi na kuchanganya kama kuwa katika ndoa au mahsian na mtu ambae hana uhakika ni nini haswa anataka. Unakuta kuna muda anaonesha kukupenda kweli, then baadae unakuta mtu huyohuyo anakufanya ujihisi hupendw. Mtu anakuacha halafu baada ya kujitahidi kuendelea na maisha yako anarudi na kukuomba mrudiane. Mtu anakwambia kabisa it's over, lakini baadae anakuita eti muyajenge. Mtu yuko na ndoa kabisa ila anajifanya yuko Single. Mtu kwa muda mfupi tu anabadilika kutoka "Nakupend sana" kwenda "nakuchukia sana". Anakufanya unajisikia vizuri kidogo tu anakubdilikia..ni mbaya zaidi kama umzaa na mtu wa aina hiyo ambae haeleweki. Itaendelea Next Post

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI: MREMBO LATIFA 12

MTUNZI: EDO MAN

Walichukua zaidi ya saa moja na nusu, wakafika Tandale Kwa Mtogole. Chumba k" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955779232077729504

HADITHI: MREMBO LATIFA 12 MTUNZI: EDO MAN Walichukua zaidi ya saa moja na nusu, wakafika Tandale Kwa Mtogole. Chumba kilikuwa shaghalabaghala, hakikuwa na mpangilio, kilionekana kwamba kwa zaidi ya mwezi mzima hakukuwa na usafi wowote uliofanyika. Nahra akashusha pumzi ndefu, muonekano wa chumba kile uliomchosha mno. Aliyaonea huruma maisha yake, hakuamini kama kuanzia siku hiyo hapo ndipo alipotakiwa kuishi. “Hapa ndiyo gheto, karibu sana mrembo,” alisema Issa huku akiachia tabasamu pana. “Mmmh! Kuzuri,” alisema Nahra, harufu mbaya ya chumbani mule, ikaanza kuiumiza pua yake. Hilo wala hakujali sana, alichokuwa akikihitaji, ni sehemu ya kuishi tu. Kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo moyo wa Deo ulivyozidi kuuma, hakuamini kama tayari msichana aliyempenda kwa moyo wote, Nahra hakuwa mikononi mwake tena. Moyo wake ulikuwa kwenye majuto makubwa, japokuwa alipewa vitisho vya kuuawa endapo tu asingemfukuza Nahra lakini kumuachia likaonekana kuwa kosa kubwa kwake kwani hata kama angemchukua na kuondoka naye kwenda kuishi sehemu nyingine, aliamini watu hao wasingeweza kumpata. Hakutaka kukaa nyumbani, alijiona kuwa na uhitaji mkubwa wa kumtafuta msichana huyo aliyeondoka nyumbani kwake usiku wa saa mbili. Alichokifanya siku hiyo ni kuondoka nyumbani, sehemu ya kwanza ambayo ilimjia kichwani mwake ni kwenda kumuulizia nyumbani kwao, Msasani.Alipofika huko, mtu wa kwanza kabisa kuonana naye alikuwa mlinzi, Chichi. “Namuulizia Nahra,” alisema Deo huku akionekana kutokuwa sawa. “Daah! Deo, hata salamu?” “Nimechanganyikiwa kidogo. Mambo vipi!” “Poa. Nahra hayupo.” “Hayupo! Si alikuja hapa jana usiku? Chichi, usinifiche bwana, mimi mweusi mwenzako, naomba uniitie Nahra,” alisema Deo huku akionekana kutokuwa sawa kabisa, alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa. “Deo, siwezi kukuficha kitu, mbona zamani nilikuwa nakuitia freshi tu. Jana Nahra alikuja hapa home, mdingi wake aliwaka kinoma, akamtimua kama mbwa,” alisema Chichi. “Unasemaje?” ITAENDELEA…

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI: MREMBO LATIFA 11

MTUNZI: EDO MAN

Alikasirika, alimkasirikia kijana huyo. Hakutaka kuzungumza chochote kile, m" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955775861518443535

HADITHI: MREMBO LATIFA 11 MTUNZI: EDO MAN Alikasirika, alimkasirikia kijana huyo. Hakutaka kuzungumza chochote kile, machozi yaliendelea kumbubujika tu mashavuni mwake. “Nini kinaendelea?” aliuliza mwanaume yule. Hapo ndipo Nahra alipoanza kusimulia kile kilichokuwa kimetokea maishani mwake tangu alipoanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Deo, alipopata mimba iliyompelekea kufukuzwa na wazazi wake na hata ndugu zake ambao hawakutaka hata kumuona. Historia ya maisha yake ilimshtua mwanaume yule aliyejitambulisha kwa jina la Issa, naye akajikuta akianza kuwachukia Wahindi. “Kwa hiyo hauna pa kuishi?” aliuliza Issa. “Sina. Sina chochote katika maisha yangu.” “Basi poa, kama vipi wapotezee tu, twende tukaishi gheto kwangu,” alisema Issa kwa lafudhi za kihuni. “Unaishi wapi?” “Tandale Kwa Mtogole.” “Mmmh!” “Nini tena?” “Gari unapandia wapi?” “Hahah! Hapa hakuna gari, tunakwenda kwa ngondi tu, tunazama hapo mbele, tunaibukia Jangwani, tukizama tena Magomeni, tunaibukia Tandale, dakika tano tu, tupo gheto,” alisema Issa huku akicheka, alikuwa akiongea maneno ya mtaani zaidi. Kutoka katika maisha ya fedha aliyokuwa akiishi, kutembelea magari, leo hii, kila kitu kilikuwa kimebadilika. Japokuwa Issa alionekana kijana mhuni asiyekuwa na chochote, lakini hakutaka kukataa kwenda kuishi kwake. Hakuwa na kitu, huyo Issa aliyeonekana kuwa mhuni, kwa matatizo aliyokuwa nayo, kwake alionekana kuwa msaada mkubwa. Hivyo akakubaliana naye na kuanza kwenda naye huko Tandale. **** Alichoka sana, kila wakati alikuwa akipumzika, jua lilimchoma mno huku akitokwa na jasho jingi. Issa hakutaka kujali, bado walikuwa wakiendelea na safari kwa miguu kama kawaida. Alipokuwa akipumzika, Issa alisimama na kumsubiri huku akimtia moyo kwamba ilibakia umbali kidogo kufika Tandale hivyo alitakiwa kuvumilia. Kwa muonekano tu, Issa alikuwa kijana masikini asiye na kitu chochote cha maana nyumbani kwake. Alionekana kupigwa mno na maisha na kila alipofikiria kama kijana huyo angekuwa msaada mkubwa kwake, moyo wake ukakataa hilo. Walichukua zaidi ya saa moja na nusu, wakafika Tandale Kwa Mtogole. Chumba kilikuwa shaghalabaghala, hakikuwa na mpangilio

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI: MREMBO LATIFA 10 Muda wote treni ilikuwa ikipiga honi lakini Nahra hakutoka relini, alidhamiria kujiua kwa kuk" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955347105997700550

HADITHI: MREMBO LATIFA 10 Muda wote treni ilikuwa ikipiga honi lakini Nahra hakutoka relini, alidhamiria kujiua kwa kukanyagwa na treni hiyo. Huku treni ikiwa imebakiza kama hatua thelathini za miguu ya binadamu huku Nahra akiendelea kulala relini pale na macho yake yakiwa yamefumba, ghafla akashtuka akishikwa mikono na kuanza kuvutwa. Hapo, akayafumbua macho yake kuangalia ni nani aliyekuwa akimvuta. Macho yake yakatua kwa kijana mmoja mchafumchafu, aliyevalia pensi ya jinzi chakavu huku mdomoni mwake akiwa na sigara. “Toka hapo, njoo huku,” alisema kijana yule huku akimvuta Nahra kutoka katika reli ile. Kwa kuwa kijana yule alikuwa na nguvu Nahra akajikuta akitolewa katika reli ile na treni kupita kwa kasi kubwa. “Unataka kujiua?” aliuliza jamaa yule huku akimwangalia Nahra machoni, alikuwa akimshangaa tu. “Ungeniacha nife, sitaki kuishi, naomba uniache nife,” alisema Nahra huku akilia kama mtoto. “Hapana. Kwani kuna nini? Mbona msichana mrembo unataka kujiua, hebu nieleze, kuna nini,” alisema kijana yule huku akimwangalia Nahra usoni. Kwake, Nahra alikuwa msichana mrembo kuliko mwanamke yeyote aliyewahi kumuona machoni mwake, kitendo cha binti huyo kutaka kujiua kilimshtua mno Nahra hakusema kitu, alibaki akilia tu. Bado moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, kiu ya kutaka kujiua iliendelea kumkamata moyoni mwake. Lawama zake zote zilikuwa kwa mwanaume huyo aliyemtoa relini, hakujua ni aina gani ya maisha aliyokuwa akiyapitia, hakujua ni jinsi gani moyo wake ulikuwa kwenye chuki kubwa dhidi ya wazazi wake na hata ndugu zake. “Kuna nini Mhindi wewe?” aliuliza mwanaume yule. “Nataka kufa.” “Kwa nini? Umechoka kula ugali?” “Hapana kaka, nataka kufa tu.” “Hebu kwanza tutoke hapa, unaweza kuniletea msala,” alisema mwanaume yule na kuanza kuondoka mahali pale. Wakatoka sehemu ile karibu na reli ile na kwenda juu kulipokuwa na daraja ambapo wakavuka na kuanza kutembea pembezoni mwa Barabara ya Kilwa huku wakielekea Kariakoo Relini. Nahra alikuwa akilia tu, alikitamani mno kifo kuliko kitu chochote kile, hakuamini kama kweli mwanaume huyo alikuwa amemuokoa na wakati alidhamiri kujiua. Alikasirika, alimkasirikia kijana huyo.

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "Hadithi:MREMBO LATIFA 09
MTUNZI: EDO MAN “Nitajiua tu,” alijisemea Nahra na kujibanza sehemu huku akisubiria treni ipiti" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955344677890146325

Hadithi:MREMBO LATIFA 09 MTUNZI: EDO MAN “Nitajiua tu,” alijisemea Nahra na kujibanza sehemu huku akisubiria treni ipitie na yeye kulala relini. Aliyachoka maisha yake hiyo ndiyo sababu iliyompelekea kutaka kujiua siku hiyo. Hakutaka kuendelea kuishi na wakati watu wote aliokuwa amewaamini hawakutaka kuishi na yeye. Moyo wake ulimuuma, hakukuwa na kitu kingine alichokiona kuwa suluhisho la maisha yake zaidi ya kujiua tu. Alidhamiria kufanya hivyo kwa kuamini kwamba asingeweza kuumizwa tena, asingeweza kulia tena, huko atakapokuwa, angeishi maisha matamu milele na kuepuka ghadhabu za dunia hii. “Pooooooo,” ilisikika honi ya treni ya mizigo, alipoisikia honi hiyo, akachungulia kwa jicho moja kutoka pale ukutani alipojibanza. Treni ile ya mizigo ilikuwa ikija kwa kasi. Ilikuwa imetoka kituoni na kuanza safari yake, alipoiona treni hiyo kwa mbali, Nahra akasubiri mpaka ikaribie na ndiyo aende kujilaza relini na hatimaye aweze kufa na kuyaepuka mateso aliyokuwa akiyapata. “Nisamehe Mungu! Mateso yamezidi, acha tu nijiue ili wazazi wangu wapumzike, wasinichukie tena. Pia nisamehe kwa kukiua hiki kiumbe unachokitengeneza tumboni mwangu. Mungu, sifanyi hivi kwa kupenda, najua unayajua maisha ninayopitia,” alisema Nahra huku treni ile ikiendelea kusogea zaidi. Nahra aliendelea kuisubiria,treni ilibakisha kama hatua mia mbili kabla ya kufika pale alipotaka kujilaza. Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo tele, alikuwa tayari kujiua lakini si kuendea kuishi kwa mateso kama aliyokuwa akiishi. “Bora nife tu, sina haja ya kuendelea kuishi,” alisema Nahra. Baada ya sekunde kadhaa, treni ilikuwa mbali kama hatua mia moja, alichokifanya Nahra, akakimbilia relini na kujilaza. Machozi yalimbubujika mashavuni mwake, hakuamini kama maisha yake yote aliyokuwa akiishi, mwisho wa siku alikuwa amefikia hatua ya kujiua. “Nisamehe Mungu, sikupenda kujiua, ila sina jinsi. Acha nife na mwanangu aliyepo tumboni,” alisema Nahra, treni ya mizigo ilikuwa ikija kwa kasi, na ilibakisha hatua arobaini tu za miguu ya binadamu kabla ya kumkanyaga pale relini alipokuwa amelala.

@simbasctanzania INAOMBA RADHI KWA MASHABIKI ZAKE WOTE DUNIA NZIMA KWA USHINDI MWEMBAMBA WALIOUPATA LEO KATIKA UWANJA WA TAIFA DHIDI YA JS SAOURA HAYAKUWA MAPENZI YETU BALI NI KUTOKANA NA KIKOKOTOOO CHA ZAMANI... TUNAOMBA CAF WATULETE BARCELONA AU MAN CITY KIDOGO KWA MCHINA PLZ @hajismanara@mwanafa@moodewji@babutale@simbasctanzania@carrymastory@baba_keagan@shaffihdauda@seekertz_@idrissultan@flavianamatata Eti Kwani Kunamtu Anateseka ???? @baraka_mpenja@ramadhaningoda

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 08
MTUNZI: EDO MAN “Nikusaidie nini?” aliuliza Mithun huku akijitahidi kujizuia kupumua kupitia pu" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955091042170031543

HADITHI:MREMBO LATIFA 08 MTUNZI: EDO MAN “Nikusaidie nini?” aliuliza Mithun huku akijitahidi kujizuia kupumua kupitia pua yake, maji yaliyokuwa yameilowanisha nguo ya Nahra, yalikuwa yakinuka. “Naomba unisamehe,” alisema Nahra huku akijitahidi kupiga magoti chini. Alikuwa akilia kwa maumivu makali, alijua kwamba alifanya makosa kumkataa mwanaume huyo aliyekuwa na lengo la kumuoa na kumkubali Deo aliyekuwa amemfukuza kama mbwa. Macho yake yalionyesha kila kitu, alikuwa akiomba msamaha lakini Mithun hakujali. Alikumbuka vema kila kitu kilichotokea katika maisha yake ya nyuma na binti huyo. Alimpenda Nahra na kuahidi kumuoa lakini maamuzi ya msichana huyo yalikuwa kwa Deo, mwanaume mweusi aliyempa mimba na kumtimua. “Unanuka Nahra,” alisema Mithun maneno yaliyomuumiza mno Nahra, ila kwa kuwa alikuwa na uhitaji, akavumilia. “Naomba unisamehe Mithun.” “Nikusamehe ili iweje? Na hicho kitumbo ukipeleke wapi? Nikusamehe wewe? Ulivyonikataa kwa maneno ya dhihaka! Nahisi umepotea njia. Kwanza unanuka sana, hivi ulioga jana?” alisema Mithun na kuuliza kwa dharau. Kilio cha Nahra kikaongezeka zaidi, hakuamini kama maneno yale yote yalitoka Mithun. Alijitahidi kuomba msamaha lakini matokeo yale aliambulia maneno ya kejeli tu, hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, akaondoka zake huku akilia. “Nitakwenda wapi mimi? Nitaishi vipi mimi? Bora nikajiue tu, siwezi kuendelea kuishi,” alijisemea Nahra na huku akipiga hatua kuelekea nje ya ghorofa hilo. Huo ndiyo ulikuwa uamuzi alioufikia, hakutaka kuendelea kuishi tena, mateso na maumivu aliyoyapitia yalitosha kabisa kumfunza, hivyo alitaka kujiua kwa kuamini kwamba angekwenda kupumzika. Akaanza kukimbia kuelekea Kariakoo Relini huku lengo lake kubwa ni kwenda Mivinjeni. Hakukuwa na kitu alichokifikiria zaidi ya kujiua tu, alitaka kuiondoa roho yake kwa kulala kwenye reli na treni kupita juu yake. Mara baada ya kufika Kariakoo Relini, akachukua Barabara ya Kilwa na kunyoosha nayo kama alikuwa akienda Bandarini. Alipofika Mivinjeni, akaanza kuelekea katika reli iliyokuwa chini ya daraja ambako kulikuwa na vyumba vingi vya reli ya kati.

Browse Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI: MREMBO LATIFA 07
Mtunzi: EDO MAN “Nitamtafuta tu,” alisema Deo huku akijipa uhakika kwamba angeweza kumuona ten" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955087855195237036

HADITHI: MREMBO LATIFA 07 Mtunzi: EDO MAN “Nitamtafuta tu,” alisema Deo huku akijipa uhakika kwamba angeweza kumuona tena Nahra aliyekuwa na mimba yake. **** Nahra alikuja kupata fahamu asubuhi, alikuwa katika majani yenye unyevuunyevu, mwili wake ulikuwa ukimuwasha. Pamoja na kuwashwa huko, alikuwa akisikia maumivu makali chini ya kitovu. Akaanza kujiuliza sababu ya yeye kuwa mahali hapo, hakukumbuka kitu chochote kile, alibaki akishangaa mpaka kumbukumbu zilipokaa sawa na kuanza kukumbuka kila kitu kilichotokea usiku uliopita, Nahra akaanza kulia, akajiangalia, sehemu zake za siri zilikuwa zimeharibiwa vibaya, akaendelea kulia mfululizo huku akijiinua kuelekea barabarani. Kila mtu alibaki akimshangaa, alionekana msichana mrembo mno lakini muonekano wake ulikuwa tofauti kabisa, alikuwa msichana mchafu mno, kwa jinsi uzuri wake ulivyokuwa, hakutakiwa kuwa kama alivyokuwa. “Hata kama nimechafuka na hata kama nimebakwa, bado ninahitaji kumuona Mithun, ni lazima nimfuate na anisaidie, sina kimbilio jingine zaidi yake,” alisema Nahra. Kila alipopita, watu walimshangaa, hakuwa akitembea kawaida, alikuwa akichechemea kama mtu aliyekanyaga mwiba. Alitembea hivyohivyo mpaka alipofika maeneo ya Fire ambapo akaunganisha mpaka Mtaa wa Twiga, mtaa uliokuwa na maghorofa mengi, huko ndipo alipokuwa akiishi Mithun. “Mungu, naomba Mithun anikubalie, anisamehe kwa kila kitu niweze kuwa naye, asahau kila kitu kilichotokea maishani mwetu,” alisema Nahra, tayari alikuwa amefika katika mlango wa nyumba ya kina Mithun, akaanza kugonga mlango, moyo wake ulijawa hofu. Wala hazikupita dakika nyingi, mlango ukafunguliwa, mtu aliyekuwa akimuhitaji ndiye aliyefungua mlango, alikuwa Mithun. Mwanaume huyo alibaki akimwangalia Nahra huku uso wake ukiwa kwenye mshangao mkubwa. Hakuamini kama yule aliyesimama mbele yake alikuwa Nahra yule aliyekuwa akimfahamu au alikuwa mtu mwingine. Alikuwa mchafu mno, nguo zake zilikusanya majanimajani huku zikiwa zimetapakaa tope, kwa kumwangalia tu, Mithun alijisikia kinyaa. “Nikusaidie nini?” aliuliza Mithun huku akijitahidi kujizuia kupumua kupitia pua yake, maji yaliyokuwa yameilowanisha nguo ya Nahra, yalikuwa yakinuka.