Browse images and videos on Instagram. Find out Most Popular Hashtags and Users.imgable
  1. Homepage
  2. itaendelea

#itaendelea photos and videos on Instagram

Medias attached with hashtag: #itaendelea on Instagram

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Browse  image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MOYO HAUNA KIFICHO 23

Licha ya kuwa mrembo sana wa sura, rangi na umbo, lakini ana moyo wa unyenyekevu na si mwenye kuk" - 1911065335836304990
Report Share Download 1 38

MOYO HAUNA KIFICHO 23 Licha ya kuwa mrembo sana wa sura, rangi na umbo, lakini ana moyo wa unyenyekevu na si mwenye kukurupuka katika kufanya maamuzi. Miezi sita imepita sasa tangu tuanze uhusiano, sijawahi kumtoa kasoro naweza sema, au pengine upendo wangu kwake umenipiga upofu. Ndani ya kipindi hiki, nimefahamiana na familia yake kwa karibu, na kumtambulisha kwa familia yangu. Nilichagua siku maalumu kumtambulisha kwa rafiki yangu Obey, ambaye kwajili ya Latiffa, tulimaliza kipindi kirefu bila kuonana (Obey alifurahi sana nilipompa mchakato mzima kuhusu kisa cha mapenzi yangu kwake). Kasi yetu imekuwa kubwa kidogo, lakini nadhani ni vema kwangu kufanya hivyo kwa binti mrembo kama huyu. Mimi si mpenzi sana wa kuandika, lakini nimetumia muda wangu kuandika kijitabu hiki kifupi, kama zawadi ya pekee kwa mpenzi wangu siku nitakayomvisha pete. natumai nitakuwa nimekamilisha kuchapisha kitabu hiki kwa ajili yake. Nafikiria kuifanya siku yetu maalumu kuwa ya kipekee sana Nitaandaa gari aina ya Limousine nyeusi, yale magari marefu sana. Gari aina hiyo, kuna ambazo mtu akiwa ndani anakuwa kama yuko sebuleni au chumbani. Nitanunua nguo nzuri sana, tukisaidiana na dada yake kuchagua, viatu pamoja na hereni za thamani, na kitu cha kuvaa mkononi, nitavifunga kama zawadi nzuri . Nitaandaa ndugu zake wa karibu, marafiki zake na ndugu wa upande wangu, bila kumpa yeye taarifa yoyote. Sherehe itaandaliwa kati ya hoteli nzuri hapa mjini, na ndugu wote watakuwa huko mida ya saa 12 jioni. Wakati huo yeye atajua niko Zanzibar, lakini nitakuwa Dar es Salaam siku hiyo tayari, na nitamtumia ujumbe akiwa ofisini kumwambia kuna mtu amemletea mzigo, dakika chache kabla ya muda wake wa kutoka, nikiweka namba ya huyo dereva wa hilo gari la Limousine, huku nahakikisha dereva ameshafika hapo ofisini. Akishuka, atampigia simu na kumpata ambapo dereva huyo atampa maelekezo ya kupanda ndani ya gari na kufungua boksi kubwa ya zawadi itakayokuwa nyuma. Akiifungua atakutana na ujumbe wa kumuomba avae kila kitu akiwa ndani ya gari, kwani dereva hataweza kumuona wala hakutakuwa na mtu yeyote (ni sawa na chumbani). Atampeleka mpaka mahala tulipoandaa sherehe hiyo #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Browse  image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MOYO HAUNA KIFICHO (22)

Niliposhuka uwanja wa ndege wa mwl. Nyerere, mtu wa kwanza kutaka kumuona alikuwa Latiffa, hivy" - 1910856063101785385
Report Share Download 1 52

MOYO HAUNA KIFICHO (22) Niliposhuka uwanja wa ndege wa mwl. Nyerere, mtu wa kwanza kutaka kumuona alikuwa Latiffa, hivyo nilichukua gari inipeleke moja kwa moja ofisini kwake. Lakini nilipita pale namanga na kutengeneza ua zuri kwa haraka na kununua kadi ya ASANTE. Kitendo cha yeye kusema ameamua kuwa namimi ni kama kilinipa funguo na ujasiri wa hali ya juu. Nikiwa na boksi ndogo ya zawadi, na kadi na ua mkononi mwangu, siku hiyo nilifika mpaka mapokezi ya ofisini kwake nikamuulizia. Sikuwa nimemjulisha kuwa ninakuja, nikikusudia iwe sapraizi. Alipigiwa simu, akajulishwa kuna mgeni wake, nikaelekezwa ofisi yake ambayo walikaa yeye na mfanyakazi mwenzie mmoja wa kike. Alifurahi mno kuniona, kwa mshangao mkubwa kwani jana yake tuu nilitoka kujilalamisha kuwa natamani sana kuja ila sitaweza kupata nafasi mpaka baada ya siku nne. “Una tabia mbaya wewe”, alisema. Mbele ya huyo rafiki yake, tulikumbatiana kwa furaha sana, nikambusu kidogo juu ya midomo yake, nikampa maua na zawadi yake nilivyokuwa nimeweka mezani kwake nilipoingia. Ndani ya kadi niliandika ujumbe mfupi,”Umenipa zawadi kubwa mno kunikubali. Asante sana”. Zawadi niliyofunga, ambayo ndiyo ilinichelewesha kuondoka Zanzibar ni cheni ya dhahabu ya hadhi ya juu, yenye jina lake, lakini mbele kuna herufi H, yaani Latiffa H, nikimaanisha Latiffa Hammy. Nilimuomba afungue hapo hapo, nikamvisha, huku nikimwambia, ikitokea ukaniacha utaenda kuiyeyusha utengeneze kitu kingine. Nilimuomba rafiki yake msamaha kwa kuwasumbua wakati wa kazi, nikamuaga Latiffa na kuondoka huku nikimsisitiza kuonana naye baada ya kazi. Mapenzi kati yangu na Latiffa yameanza, mahaba mazito sana kati yetu. Nampenda kuliko nilivyowahi kupenda kabla, nampenda kuliko nafsi yangu nahisi. Niko tayari kufanya lolote kwa ajili yake. Sifikirii maisha bila yeye. Baada ya kuwa naye, nimegundua vitu vingi sana ndani yake, vinavyonifanya kumpenda zaidi. Yeye ni mchangamfu, mchapakazi na binti mwenye maono na malengo makubwa. Licha ya kuwa mrembo sana wa sura, rangi na umbo, lakini ana moyo wa unyenyekevu na si mwenye kukurupuka katika kufanya maamuzi. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Browse  image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MOYO HAUNA KIFICHO 21

lakini hata siku moja hakunitamkia neno lolote kunionesha kwamba naweza kuwa nimeanza kuchukua na" - 1910713873276913326
Report Share Download 2 64

MOYO HAUNA KIFICHO 21 lakini hata siku moja hakunitamkia neno lolote kunionesha kwamba naweza kuwa nimeanza kuchukua nafasi moyoni mwake. Niliridhika kuwa rafiki wa karibu, nilifarijika kukaa naye, kula naye, kucheka na kuzungumza na huyu mwanamke niliyempenda sana. Ilinilazimu kurudi Zanzibar baada ya siku nane, hivyo siku ya saba jioni tulikaa kwenye mgahawa mmoja wa kimahaba, maeneo ya masaki, kuwa na muda mzuri wa kuagana. Baada ya maongezi ya muda mrefu, kama kawaida yangu, nikajipendekeza, nikajisogeza karibu kabisa na Latiffa na kuanza kumwambia jinsi ninavyojisikia kuwa karibu naye. Mara zote huwa nikimwambia hayo maneno, yeye hutabasamu tuu na kusema asante wakati mwingine, lakini, siku hiyo alinishangaza. Nilipoongea nae huku mkono wangu wa kulia umeshika bega lake, alinigeukia na kunitizama machoni, kisha akaniambia kwa lugha ya kiingereza,”I think I love you Hammy”, akimaanisha, “Nadhani nakupenda Hammy”. Kidogo nichanganyikiwe siku hiyo, kwa furaha. Niliinuka, nikamshika mkono, nikamuomba arudie hicho alichosema tukiwa tumesimama. Akarudia tena, “Nadhani nakupenda”. Nikiwa nimemuangalia usoni, nilianza tena kujieleza,”Sitaki kujua kama hicho unachodhani ni kweli au si kweli. Inatosha kudhani unanipenda, nitakusaidia kujua kuwa unanipenda kweli mpenzi, nashukuru sana kwa kuwa muwazi kwangu.” Hapo nilimkumbatia kwa nguvu sana huku nikimshukuru na kumueleza jinsi ninavyompenda sana. Sikutamani muda uende, sikutamani niondoke kesho yake, sikutamani siku hiyo iishe. Nafsi yenye kiu ilikuwa inapata maji bariidi, wakati wa jua kali. Tulikaa muda mwingi zaidi usiku huo, mpaka saa nane usiku, nikamrudisha kwake nikarudi kupumzika kwa ajili ya safari. Wiki chache baadaye, nikiwa Zanzibar, huku tukiendelea kuwasilianza, Latiffa alinitamkia kwenye simu kuwa amefanya maamuzi ya kuwa na mimi na hatageuka. Hii habari ilikuwa njema mno hivyo sikutaka niisikie kwenye simu tuu. Nilipanga safari baada ya siku mbili, kuja kuipokea rasmi habari ya kukubaliwa. Niliposhuka uwanja wa ndege wa mwl. Nyerere, mtu wa kwanza kutaka kumuona alikuwa Latiffa, hivyo nilichukua gari inipeleke moja kwa moja ofisini kwake. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Browse  image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MOYO HAUNA KIFICHO 20

Nilijua najiweka hatiani kutaka penzi kwa binti ambaye pengine moyo wake bado umebeba mtu mwingin" - 1910701710667714508
Report Share Download 1 63

MOYO HAUNA KIFICHO 20 Nilijua najiweka hatiani kutaka penzi kwa binti ambaye pengine moyo wake bado umebeba mtu mwingine, nilifikiri endapo mpenzi wake wa awali akimbembeleza wakarudiana nitakuwa kwenye hali gani. Lakini kwangu faraja ya Latiffa ilikuwa muhimu. Sikutaka awe na huzuni japo pia nilitumia fursa hiyo kujiweka karibu. Labda bahati ingeniangukia, akanipenda mimi moja kwa moja. Usiku ule ulikuwa wa kipekee sana kwangu, nilimrudisha Latiffa saa nne na nusu usiku, alipotaka yeye, kwani angeniruhusu tungekaa mpaka asubuhi. Wakati tunaarudi alikuwa amerejea katika hali ya uchangamfu hivyo nikajipongeza kuwa kazi nimeifanya vizuri. Tulifika kwake, nikashuka na kuja upande wake. Si kuwa nina tabia za kizungu sana, kumfungulia mwanamke mlango wa gari, au nataka kujionesha hivyo kwa Latiffa, ila niliona hiyo ndiyo njia rahisi ya kupata kumbato lake kwa mara nyingine tukiwa tumesimama. Alishuka kwenye gari, nikashika mikono yake miwili, nikamvuta karibu na kumkumbatia kwa nguvu sana. Mara hii hakunizuilia mapema, basi nikakaa pale kama dakika nzima au zaidi. Nadhani unaelewa hisia zilizoendelea ndani yangu wakati huo, yani nilitamani kuendelea kumuweka kifuani kwangu hata kwa saa nzima, lakini hilo lisingewezekana. Tuliagana, akaondoka. Niliporudi hotelini, baada ya kuoga na kuingia kitandani, nilimpigia simu kumuuliza kama amelala tayari. Sikuwa na cha kumwambia hasa, lakini nafsi yangu ilifurahi kumsikia kwa simu. Usiku kucha nilimuwaza Latiffa, nikiwaza tulivyokumbatiana na nilivyojihisi, niliwaza huzuni aliyokuwa nayo na nilivyotumia fursa ile kujiweka karibu, niliwaza alivyotabasamu, niliwaza alivyolitamka jina langu, yani kila kitu mpaka alivyokosa cha kuniambia. Nilijifariji kuwa ameanza kunipenda na ndio sababu amenitoa Zanzibar ili nikae naye tuu wakati anapitia ugumu kwenye mahusiano yake. Nilitamani kesho yake ifike haraka nimtafute tena, nimuombe kuonana. Wiki hiyo nzima Latiffa alinipa nafasi ya kuonana naye kila siku, tukiwa na wakati mzuri wa pamoja jioni, tukitembelea maeneo tofauti tofauti, lakini hata siku moja hakunitamkia neno lolote kunionesha kwamba naweza kuwa nimeanza kuchukua nafasi moyoni mwake. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Browse  image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MOYO HAUNA KIFICHO 18

Mvua ikiendelea kunyesha, alinivuta kunionesha tunatakiwa kuondoka eneo hilo, tukaelekea sehemu a" - 1910101179440182797
Report Share Download 3 63

MOYO HAUNA KIFICHO 18 Mvua ikiendelea kunyesha, alinivuta kunionesha tunatakiwa kuondoka eneo hilo, tukaelekea sehemu ambapo mvua haifiki, lakini sote wawili tukiwa tumelowa kiasi. Nilimuhurumia kuwa angesikia baridi, hivyo haingekuwa sawa kukaa na nguo mbichi. Nilimuomba tuondoke hapo hotelini, tukaondoka, nikampitisha kwenye duka moja la nguo, nikamnunulia gauni simpo, nikamuomba twende hoteli niliyofikia. Nilimpa funguo ya chumba changu, akaingia kubadili nguo huku nikimsubiri kwa nje, halafu nami nikaingia kubadili alipotoka, nikavaa kinyumbani zaidi yaani pensi na tisheti na viatu vya wazi. Tulipanda juu kwenye mgahawa, tukaagiza kahawa na kuanza kunywa. Nilitamani Latiffa aanze kuzungumza, lakini niliogopa kumuharikisha kwani sikuwa najua nini hasa angetaka kuniambia. Muda si mrefu, alianza kuongea Uliniuliza kuhusu mahusiano yangu, sikutaka kuzungumzia. Lakini mara ya pili tunaonana nilikuwa na mpenzi wangu, hilo unajua. Yule mwanaume nilimpenda sana, na nilitegemea tungeoana. Wakati ule alikuwa ametoka masomoni, ni mwanajeshi, hivyo alipokuwa masomoni kwa muda mawasiliano hayakuwepo kabisa, muda wa kama mwaka mzima, lakini alipokuja tuliendelea na sikuwahi kuwa na mwanaume mwingine kwa kipindi kile chote. Tulikaa huku nikitegemea tuanze taratibu za kuoana kwani uhusiano wetu tayari ulifikisha miaka mitatu wakati huo, lakini yeye alikuwa mzito kidogo. Baada ya kuvutana kiasi, alinivisha pete kwa mshtukizo yaani sapraizi, kabla hata hajatoa barua ya posa. Sikufurahia sana kile kitendo, japo yeye alidai kuwa ni hatua kubwa sana katika kuoana. Tulikaa kama miezi sita bila kuendelea na hatua yoyote. Sasa wiki kadhaa zilizopita nimepata habari kuwa ana mtoto aliyemzaa na mwanajeshi kipindi yuko masomoni, na mama yake amekuja hapa mjini kumtafuta. Nimefatilia nikajua ukweli, japo mwanzo nilimuuliza akakataa kabisa, lakini baada ya kubaini ukweli amekubali na kuanza kuniomba msamaha. Mbaya zaidi huyo mwanamke nahisi bado wanaendelea na mahusiano. Juzi kati, tukiwa kwenye huu mgogoro, alipiga akidai kuwa sitaki kumsamehe kwakuwa nimepata mwanaume mwingine. Kuna kitu aliwahi kufanya kipindi cha nyuma tukagombana sana, #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Browse  image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MOYO HAUNA KIFICHO (17)

Nilimpigia kijana wangu, kumuomba afike nyumbani saa kumi alfajiri, akanisindikiza uwanja wa nd" - 1910089398957284318
Report Share Download 0 42

MOYO HAUNA KIFICHO (17) Nilimpigia kijana wangu, kumuomba afike nyumbani saa kumi alfajiri, akanisindikiza uwanja wa ndege, nikampa na maelekezo muhimu ya biashara, nikaondoka. Niliwaza ni nini hasa binti huyu anataka kuniambia, kwa dharura ya namna hiyo. Nilijipa moyo kwamba hawezi kunisumbua, kunitoa Zanzibar kama hana jambo la msingi la kuniambia, lakini sikutaka kuweka matumaini kwamba atakuwa ananikubali. Ni siku chache tuu, nilipata simu kunithibitishia kuwa yuko kwenye mahusiano, na haingekuwa rahisi hata kidogo kunipa nafasi mimi pia. Hata hivyo, wito wake ulikuwa muhimu mno kwangu. Jioni ilifika, nikamfata kazini mapema kidogo, kwani alitaka nimfate saa tisa. Tulipoonana, nilishuka kwenye gari kumpokea, nikamshika mkono, nikajikuta nimemvuta kumkumbatia. Nadhani nilichohitaji ni kumkumbatia, nijifariji kwa uwepo wake karibu yangu. Sielewi ujasiri huo niliupata wapi, lakini nashukuru hakukataa kumbato langu, japo hakuniruhusu kuendelea kwa muda mrefu. Tuliingia kwenye gari, na siku hiyo sote hatukuwa wachangamfu kama awali. Tulizungumza tuu mambo ya msingi, hakukuwa na utani wowote kati yetu. Nilimuuliza kama alikuja na gari, akasema alikuja nalo lakini amemuachia rafiki yake funguo hivyo tunaweza kuondoka pamoja. Akili yangu wakati huo iliwaza, kama Latiffa angeniambia huu ndio mwisho wetu, sijui ningefanyaje. Nilihisi kumpenda kuliko nilivyowahi kupenda kabla. Tulienda hoteli fulani kubwa, iliyo kando mwa bahari, tukakaa sehemu ya wazi jirani na maji. Tukiwa tumeagiza vinywaji, ghafla mvua ilianza kunyesha, hizi mvua za Dar zinazokuja bila taarifa. Tulipokaa hapakuwa na mwanvuli juu, palikuwa wazi tuu, mbali kidogo na majengo ya hoteli. Tuliinuka sote kwa haraka, nikamshika mkono ili tukimbie kujikinga na mvua, lakini badala ya kukimbia, tulijikuta tumesimama pale kwa muda kiasi tukitazamana, huku mvua kubwa ikinyesha. Nilimtazama machoni, nikiashiria nataka anitazame pia, zikapita sekunde kadhaa, nikamwambia,’nakupenda sana Latiffa, nakupenda’. Mvua ikiendelea kunyesha, alinivuta kunionesha tunatakiwa kuondoka eneo hilo, tukaelekea sehemu ambapo mvua haifiki, lakini sote wawili tukiwa tumelowa kiasi. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Browse  image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MOYO HAUNA KIFICHO 14

Sasa hapa sikuelewa kama labda ana mpenzi mwingine ambaye hawezi kumuacha hivyo sina nafasi kabis" - 1909482966301957349
Report Share Download 3 52

MOYO HAUNA KIFICHO 14 Sasa hapa sikuelewa kama labda ana mpenzi mwingine ambaye hawezi kumuacha hivyo sina nafasi kabisa, lakini ananihurumia kunikatisha tamaa, au labda ananichunguza kwanza kabla ya kunikubali, au pengine ana mpenzi lakini haoni kesho naye lakini bado hawajaachana, au ni vipi. Ila mbali na yote, ilitosha kunipa nafasi ya urafiki. Nikiwa Zanzibar, niliendelea kuwasiliana na mrembo wangu, na niwe muwazi, nilifika mahala nikasahau kama bado hajanikubalia, mpaka siku nilipopokea simu ya mwanaume wiki kama tatu baadaye. Huyu mwanaume hakujitambulisha jina lake, lakini alisema ni mpenzi wa Latiffa , ambaye hivi karibuni amegundua namfatilia sana. Nilishindwa cha kumjibu yule jamaa, nikabaki kimya kwa sekunde halafu nikakata simu. Bila mimi mwenyewe kujielewa nilihisi machozi yananitoka. Mwanamke, kwa mara ya kwanza, alinitoa machozi ya uchungu, hii ilikuwa kama ndoto. Wakati huo nikiwa kwa mteja wangu mmoja, nimesimama pembeni kuongea na simu hiyo, nilibaki hapo kwanza, nikitafuta pozi la kuwa sawa tena. Nilifanya haraka kumuaga mteja, nikamuachia gari ya mizigo kijana aendelee na kusambaza mizigo kwa wateja huku nikisingizia kichwa kinauma, nikarudi nyumbani kwangu haraka sana. Chumba changu nimekitengeneza kwa namna ya kunipa mapumziko haswa, yani nikishafika chumbani kwangu hua kiasi fulani msongo wa mawazo unapunguzwa na yale mazingira ya chumba tuu. Rangi za chumba, aina ya kitanda, kiyoyozi, tv ya kisasa, kapeti ya manyoya na ukubwa na mpangilio wa chumba vinafanya muonekano wake uwe mzuri sana. Na nilifanya hivyo sababu chumbani ndipo mahala natumia muda zaidi, hasa ninapomaliza kazi zangu zinazonifanya kuwa bize na wakati mwingine mchovu sana. Nilijilaza kitandani kama saa nzima huku nikitafakari na kuumia sana, bila kujua nini cha kufanya. Nilishindwa kujizuia kulia, na kuwaza sana, huku moyo ukiuma kama kidonda. Sikufikiri kingine chochote zaidi ya kupoteza ndoto za kuwa na Lattifa, jambo ambalo akili yangu haikuwa imelitegemea. Niliumia mno, ukizingatia mpaka wakati huo sikuwa bado na jibu lolote la Latiffa kuhusu ombi langu. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Browse  image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MOYO HAUNA KIFICHO (12)

Nilikubaliana naye, tukaendelea na mazungumzo, lakini kila wakati mazungumzo yangu yalielekea k" - 1909366571102761406
Report Share Download 2 50

MOYO HAUNA KIFICHO (12) Nilikubaliana naye, tukaendelea na mazungumzo, lakini kila wakati mazungumzo yangu yalielekea kulekule. Nilimuuliza habari zake za mahusiano ambazo hakuwa tayari kuniambia, akanieleza kwa kifupi tuu na kubadilisha mada. Tulipoendelea kukaa, niligundua si msichana mkimya kama ambavyo nilihisi mwanzo. Alianzisha stori za kunichekesha na kunishangamsha kwa namna fulani kwani jibu lake lilinifanya nipooze. Siku hiyo tulijikuta tukitumia masaa mengi kuongea kuliko nilivyotarajia. Kufika muda wa kuondoka, nilishangaa kuangalia saa yangu na kuona muda umeenda sana, kwani nilipokuwa nikiendelea kuzungumza na Latiffa nilihisi kama tumeongea kwa muda mfupi tuu. Uwepo wake ulinipa raha ya ajabu, na uchangamfu wake ulinifanya nimpende zaidi. Kufika saa tano usiku aliangalia saa na kusisitiza tuondoke. Nilitamani kuendelea kukaa, lakini sikuwa na namna ya kupinga. Ilikuwa fursa ya pekee, kupata chakula cha jioni na msichana aliyeupendeza moyo wangu sana, na kuwa na mazungumzo naye kwa urefu. Nafsi yangu iliridhika kwa kiasi. Sikuwaza tena kuwa nimejieleza bila kupewa jibu lolote. Nilimrudisha nyumbani na kurudi hotelini, lakini nilihakikisha nimemuomba kuonana tena siku nyingine. Hakunipa jibu la uhakika wa siku ya kuonana, lakini nilijipa moyo kuwa huo ulikuwa mwanzo tuu wa kuonana mara kwa mara. Usiku wa siku hiyo nadhani nililala masaa matatu kama si mawili. Nilimuwaza Latiffa, wakati wote. Nilijenga magorofa hewani naweza sema, nilijiona nikiwa naye katika mapenzi mazito, nikajifurahia. Nilitamani kumuomba anijibu kama amenikubali, tuanze mahusiano kwa haraka. Akili yangu haikunipa jibu lingine lolote zaidi ya kukubaliwa. Sikutaka kujipa mawazo tofauti na hayo, kwani yangenikosesha raha. Asubuhi kitu cha kwanza akilini mwangu ilikuwa ni Latiffa. Nilitaka kumpigia simu, nikasita kidogo nikikumbuka kuwa atakuwa anajiandaa kwenda kazini. Mara nyingi sipendi kutumia ujumbe wa simu, kwani ni mvivu wa kuandika kidogo, pia huwa najistukia nini cha kumuandikia mtu, hasa katika hali kama hiyo ya mahusiano ambayo bado hayana muelekeo wa kueleweka. Nikashika simu na kuiacha, mara mbili, lakini badae nikaamua nipige kumsalimu tuu, #itaendelea